Waziri wa Habari, Michezo na Sanaa Mhe. Dkt Harryson Mwakyembe ameitaka jamii kutunza na kuyaendeleza maeneo yote yenye Mali kale na Utamaduni wa asili ili yaendelee kuwepo kwa Vizazi vijavyo. Hayo ameyasema Waziri huyo katika Kijiji cha Masware kata ya Magugu Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara katika Ziara yake ya Kikazi Siku ya Pili kutembelea shughuli mbalimbali za Wizara yake. Akiwa katika Kijiji Masware amejionea Chechem ya Maji moto na kichuguu cha Volcano tuli ambapo amewashukuru wananchi wa Kijiji hicho kuyatunza kwa miaka mingi na akawataka wananchi hao kupanda miti ili kutunza mazingira.
Halmashauri ya wilaya ya Babati
Anwani: P.O BOX 400, Babati.
Simu ya mezani: Simu Na. 027-2531011
Simu ya Kiganjani: 0620444641,075486577
Barua pepe: info@babatidc.go.tz,ded@babatidc.go.tz
Copyright ©2020 Babati District Council . All rights reserved.